YOUTUBE PLAYLIST

Friday, March 19, 2010

Mheshimiwa mchango wako ni muhimu

Nimekuwa najaribu kumshawishi Mheshimiwa mmoja ambaye alikuwa Waziri kwa muda mrefu na sasa ni Mbunge atoe mchango katika blog hii, Mheshimiwa huyo katika miaka ya sitini alirekodi nyimbo moja nzuri sana ya kumsifu Mwalimu Nyerere. Mheshimiwa huyo alirekodi kibao hicho wakati akisoma Uholanzi.
Pia Balozi mmoja maarufu aliyekuwa akiimba nyimbo za James Brown miaka hiyo najaribu kumwomba ruksa atusaidie experience zake.
Mzee moja marehemu sasa lakini ana watoto wengi wanamuziki, japo yeye alikuwa mwalimu Tabora school alinieleza kisa cha Mheshimiwa mmoja (Mbunge muhimu), ambaye nitamwomba ruksa yake nitaje jina lake baadae, ambaye alilazimika kuwa anamlimia kajibustani kake ili afundishwe gitaa. Nashukuru kuwa mheshmiwa huyo mpaka sasa ni msaada mkubwa sana katika fani ya muziki hasa wa dini

3 comments:

  1. Anonymous19:06

    Mkuu,

    Wapo waheshimiwa kadhaa ambao aidha walikuwa wapiga ala, waimbaji au mashabiki wakubwa sana wa muziki wa dansi. Yupo muheshimiwa mmoja kwenye kabineti ya awamu ya nne alikuwa shabiki namba moja wa Sunburst na mdau mkubwa wa miziki ya disco. Tulikuwa tukitoka shule lazima tuimbe miziki yote latest.

    ReplyDelete
  2. tUTASHUKURA KAMA UTAWEZA KUMSHAWISHI ATKUMBUKE MACHACHA YA WAKATI HUO

    ReplyDelete
  3. Patrick Tsere22:54

    Yes. Talking about sunburst!!Mwaka 1984 nilienda kufanya kazi ubalozini jijini Lusaka, nilikutana na James Mwaipungu ambaye alienda kupiga na kundi lake. Kundi hilo lilisambaratika na James akabakia nchini Zambia kama mkazi na msanii. Kuna wakati alikuwa anahitaji fedha akaja kuniona nimkopeshe kiasi cha fedha ambacho hakikuwa kikubwa sana. Akaamua kuniachia gitaa lake la umeme kama rehani. Nilipokataa akaliacha pale ofisini kwangu na akaondoka na hela.

    Hayo ndiyo maisha ya wasanii wa kitanzania. Ni paradox haswa. Wanapiga muziki mzuri ambao jamii iko tayari kuulipia lakini masikini wasanii hao wanaendelea kuwa duni. Wako wengine wanapiga muziki kama hobby lakini riziki yao inatokana na shughuli nyingine. I remember marehemu Salum Abdalah yeye alikuwa full time contractor tena akimiliki idadi kadhaa ya matipper hadi anafariki. Kweli John mnayo changamoto kubwa. Ushauri wangu do not give up endelea kupigania haki zao.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...