YOUTUBE PLAYLIST

Wednesday, March 3, 2010

Bendi za wanafunzi mashuleni


Katika miaka ya sitini na sabini shule nyingi za sekondari zilikuwa na Bendi (bendi ya magitaa), hata pale Chuo Kikuu Mlimani palikuwa na Bendi nzuri tu katika kipindi hicho, Kuna Bendi za shule nyingine zilipata umaarufu wa Kitaifa kama vile Bendi ya Shule ya Sekondari Kwiro ambayo iliweza kurekodi nyimbo zake Radio Tanzania. Niongelee shule moja nadhani itatoa changamoto ya kupata habari za bendi za namna hiyo katika shule nyingine. Pale Mkwawa high School Iringa ,kulikuwa na bendi mbili. Moja ilikuwa ikipiga muziki wa kiswahili ambayo ilikuwa na wanamuziki kama Sewando kwenye solo, Masanja kwenye rythm, John Mkama Bass,Manji,Danford Mpumilwa mwimbaji, mpiga tumba kwa sasa ni Askofu moja mashuhuri, wakati huo huo bendi ya pili ilikuwa na mwimbaji machachari Deo Ishengoma akiimba nyimbo za James Brown. Bendi hii ilikweza kurekodi RTD pia vibao kama Wikiendi Iringa na Ulijifanya lulu na kadhalika.

Dar Es Salaam pia palijaa bendi nyingi za shule na mitaani. Azania, Tambaza ni kati ya shule zilizokuwa na bendi za vijana katika enzi hizo, wakipiga muziki Jumapili mchana ukiitwa bugi. Bahati mbaya bugi lilipigwa marufuku na kuharibu mfumo mzima wa muziki wa vijana katika historia ya muziki Tanzania. (Pichani ni shule ya Mkwawa wakati huo.)


10 comments:

  1. Anonymous13:42

    Yeah miaka ya sitini hata pale Dodoma Secondary School kulikuwa na Band iliyoitwa Tom Duli, kiongozi wa band hii alikuwa Patrick Balisidya, ambaye baadae alikuja kuwa mmoja wa vinara wa muziki wa hapa bongo.

    ReplyDelete
  2. mkuu nimefurahi kwa kutukumbusha kuhusu bendi za muziki shuleni, siku hizi bendi za muziki shuleni unaweza kuzikuta kwenye shule za jeshi tu kama jkt mgulani, makongo nk. Mkuu pia nilikuwa nakushauri uweke e-mail yako wazi ili iwe pia njia nyepesi ya kuwasiliana. Mwisho nimesikia upo hapa marekani, Je umefikia Maryland sehemu gani? swali kutoka kwa dj luke ambaye mmefanya kazi wote DSM ushirika club simu 2405959874

    ReplyDelete
  3. Haya mkuu email nimeweka wazi, ni jkitime@gmail.com.ratiba inanionyesha kuea katika wiki mbili zijazo tutakuwa maeneo ya Roanoke,VA,Fredrick, MD.Atlanta GA, Orlando,Ft pierce,Jacksonville FL. Naahidi ntakupigia simu.

    ReplyDelete
  4. Patrick Tsere08:15

    John Yes. Nikiwa Azania Secondary mwaka 1966 hadi 1969 mimi na wenzangu kama akina Wema Mwinyimbegu (sasa ni mwalimu shule ya Al Muntazir Upanga) tulifundishwa kupiga gitaa na mwalimu wa Muziki aitwae Martin Longfellow Mugarula ambaye baadae alihamia Finland. Kikundi chetu tukijiita the Blues kazi yetu ilikuwa kutembelea kumbi za dansi hasa pale walipokuwa Kilwa Jazz ina perform na kuvizia wakati wa interval na tukiomba 'lift' na sisi tunapiga japo kwa kujaribu jaribu.

    Nilipoenda Form V Mazengo tukaanzisha kikundi chetu tukiwa na Simon Jengo kwenye Microphone,marehemu Profesa Jumanne Hamisi Wagao bass guitar, Petro Petro Kime solo na mimi nikipiga rythm. Kwa kweli vyombo tuliazima na tukavikarabati kwenye maabara yetu pale shuleni kutoka Central Jazz bendi iliyokuwa imekufa.

    Tulikuwa tukipiga wakati wa social evenings na mapatna kutoka Msalato. Nakumbuka kabla ya hapo muziki ulikuwa wa changer. Aliekuwa Social Prefect wetu alitupinga kwa kutuwekea mtimanyongo tusipige. Tukambembeleza tupige kawimbo kamoja tu. Wee ikawa kosa. Kwani baada ya kale kawimbo kamoja wasichana wa Msalato walipofuatwa kwa ajili ya kucheza muziki wa changer walikataa. Na hata wanafunzi wenzetu wa Mazengo wakapiga kelele 'bila ya muziki wa akina Jengo hachezi mtu hapa'. Kuanzia hapo tukawa accepted. Hizo ndiyo zilikuwa enzi hizo mzee

    ReplyDelete
  5. Anonymous13:00

    Kitime umenikumbusha mbali sana wakati huo mimi nilikuwa nasoma Iringa Girls,bendi ya Mkwawa ilikuwa machachari kweli, akina Deo Ishengoma, Mpumilwa, John, Hiza na wengine wengi. Wengi wetu sasa tunaitwa babu/bibi

    ReplyDelete
  6. Kulikuwa na bendi ya fans wa Bar Keys waliojiita Bar Locks, majina yao ni pamoja na Abraham Kessy (Mjema),Nkondo Chirwa, Dorothy Macha. Wengine nimesahau majina yao, kwani ni kipindi kiasi.

    ReplyDelete
  7. Barlocks sijui kama ni hii unayoongelea au nyingine ilikuwa ya Magoa wakiishi pale katika ghorofa lilikuwa linaangliana na Printpak zamani, jirani na Maktaba Kuu, hawa walikuja kuwa Mionzi, picha zao nyingine wamenitumia, nitazitundika karibuni

    ReplyDelete
  8. Wa Iringa Girls nikukumbushe pia kuwa mlikuwa mnaitwa Zoo, kwa kuwa Jumapili mchana ndo tulikuwa tunaruhusiwa kuja kuwaangalia. Na katika wimbo mmoja wa Mkwawa, ulikuwa na kibwagizo hiki.....Dan wapi leo ni garden au zoo, ndio wikiendi, ndio wikiendi... garden hapa ni ule uwanja uliokuwa mzuri wenye viti mbele ya manispaa Iringa, palikuwa ndo mahala pa vijana kukutana siku ya Jumapili. Loooooooh

    ReplyDelete
  9. Anonymous22:33

    Nakumbuka Mkwawa High School kulikuwa na bendi mbili kama ulivyosema. Nawakumbuka kina Danfod, Masanja, Manji. Pia nakumbuka kuwa ile band ya soul ilikuwa ikiitwa Midnight Movers isipokuwa katika band hiyo nawakumbuka Marehemu Michael Kafumba , Martin Mhando na jamaa mwingine (half-caste) ambae jina lake silikumbuki. Naomba wenye kumbukumbu kali mnirefresh kumbukumbu yangu. Ex-Mkwawan.

    ReplyDelete
  10. Anonymous01:32

    Mkuu,

    Hiyo Barlocks aliyoitaja WIM ndiyo Barlocks original walikuwa balaa kama Barkeys. Abraham "Vingoko" Kessy yupo Same niliongea naye December 2009.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...